Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amesema serikali imekamilisha ujenzi wa soko kuu la wafanyabiashara mjini Katesh na kuwataka wafanyabiashara hao kuhamia kwenye soko hilo jipya lilojengwa na serikali baada ya soko la zamani kuharibiwa na maporomoko ya mawe na tope mwaka jana kutoka Mlima Hanang.

Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi wa soko hilo Rc Sendiga ametoa maelekezo ya serikali kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Hanang ikiwemo kusimamia zoezi la wafanyabiashara kuhamia katika soko hilo jipya kwani miundombinu muhimu ya soko hilo imekamilika.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *