Imeelezwa kuwa ujenzi wa daraja linalounganisha mitaa ya Ayaingi na Ayamaami kata ya Ayamaami itaondoa adha ya usafiri iliyokuwepo na kurahisisha shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wakazi na watumiaji wote.
Hayo yamesemwa na wakazi na watumiaji wa kata hiyo iliyopo Halmashauri ya mji wa Mbulu mkoani Manyara walipozungumza na kituo hiki wakati wa ujenzi wa daraja hilo.
Naye mwenyekiti wa Mtaa wa Ayaingi Nada Qwaray amekiri uwepo wa adha mbalimbali kwa wananchi wake kutokana na ukosefu wa daraja bora, na kutoa wito wa matumizi mazuri, ushirikiano na utunzaji wa miundombinu katika maeneo yao.