Katibu wa NEC itikadi uenezi na mafunzo wa CCM Paul Makonda amehitimisha ziara yake mkaoni Manyara kwa kutembelea wilaya ya Hanang ambayo mwishoni mwa mwezi Dec 2023 ilikumbukwa na maporomoko ya matope kutoka mlima Hanang.
Muenezi Makonda amesikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzitatua kwa kushirikiana na viongozi wa serikali wa mkoa wa Manyara.

Aidha makonda baada ya kuhitimisha ziara yake wilayani hanang katika mkoa wa Manyara tayari amekwisha kuwasili Mkoani Singida Ikiwa ni Mwendelezo wa Ziara zake ambazo anazifanya kwenye Mikoa Kumi ya Tanzania Bara.

Akiwa Mkoani Singida Makonda amesikiliza pia Kero za Wananchi katika Mkutano ambao umefanyika katika Viwanja vya Stendi ya Zamani Mjini Singida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *