Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amekabidhi piki piki 66 kwa jumuiya za maji katika wilaya zote za mkoa wa manyara ili kurahisisha utendaji kazi kwa watumishi hao.
Akizungumza baada ya kukabidhi piki piki hizo Sendiga amewataka watumishi hao kuzitunza piki piki hizo kwani ni Mali ya serikali ambapo amepongeza wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini ruwasa mkoa wa Manyara kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya ya kusambaza maji vijijini.
Kwa upande wake meneja wa Ruwasa Mkoa wa Manyara Injinia Wolter Kilter, amesema lengo la watumishi hao kupewa pikipiki hizo ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa uharaka zaidi.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Remidius Mwema amesema atasimamia na kufatilia kama watumishi waliokabidhiwa piki piki hizo wanafanya kazi Kama ambavyo serikali imekusudia kwani piki piki hizo zitasaidia kurahisisha usambazaji wa maji.