Mwenyekiti wa bodi ya RUWASA taifa Ruth Kayo amesema mpango wa uchimbaji visima 900 nchini una lenga kujenga visima 5 kwa kila jimbo ili wananchi wapate maji safi na salama.
Amayasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa vijiji vya Gisambala na Kinyamburi wilaya ya Hanang Mkoani Manyara katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mpango wa uchimbaji wa visima hivyo
Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha kila mwananchi ambaye hajafikiwa na huduma ya maji kufikia desemba 2024 awe amefikiwa na huduma ya maji.
Wilaya ya Hannang ni miongoni mwa wilaya zitakazonufaika na mradi huo wa uchimbaji wa visima 900 ili kuweza kupata huduma ya maji.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema hakuna mwananchi atakayeguswa na mradi unaotekelezwa na Serikali asilipwe fidia.
Ingawa inaweza kuchelewa, amesema Serikali itahakikisha inampa kila mwananchi haki yake anayostahili.
Rais Samia ametoa hakikisho hilo la fidia kwa wananchi wakati akijibu ombi la Mbunge wa Madaba (CCM), Dk Joseph Mhagama aliyeomba wananchi watakaopitiwa na ujenzi wa Barabara ya Makambako walipwe fidia.
Rais Samia amesema hayo alipozungumza na wananchi wa Madaba mkoani Ruvuma, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku sita mkoani humo aliyoianza jana Jumatatu