HOSPITALI YA HALMASHAURI YA MJI WA MBULU

Mganga mfawidhi hospitali ya halmashauri ya mji wa Mbulu mkoani Manyara Dr Deogratius Mazengo, ameishukuru serikali kwa awamu ya pili ya madaktari bingwa waliofika kutoa huduma za kibingwa katika hospitali hiyo.

Akizungumza na kituo hiki hivi karibuni mganga mfawidhi Dr Mazengo amesema ujio wa madktari hao umewarahisishia wagonjwa kupata huduma za kibigwa kwa wakati.

Amesema mwezi wa tano madaktari wa mama samia walifika lakini kutokana na wingi wa wagonjwa hawakuweza kuhudumiwa wote na hivyo kufanya utaratibu wa kuomba tena madaktari bingwa kwa ajili ya kutoa huduma.

Mganga mfawidhi mazengo Ameendelea kutoa wito kwa wagonjwa pindi wanaposikia huduma hizo za kibingwa wajitokeze kwa wingi ili kupunguza gharama za kwenda hospital za rufaa.

 

SIMANJIRO- MANYARA

Mkuu wa mkoa wa Manyara Qeen Sendiga  amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia miradi ya serikali kuwa waadilifu katika usimamizi wa kazi hizo.

Ametoa tamko hilo wakati alipokuwa akikagua miradi inayoendelea katika wilaya ya simanjiro baada ya kubaini kufanyiwa udanganyifu kwa kuwaandaa watu kwenda kufanya kazi baada ya kugundua kuwa mkuu wa mkoa anaenda kufanya ukaguzi.

Mkuu wa Mkoa Sendiga ameonesha kutokuridhishwa na mradi wa ujenzi katika shule ya sekondari Songambele wilayani Simanjiro na kubaini ujenzi ulisimama kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa Mradi wa bweni kwa ajili ya walemavu katika shule hiyo ya Sekondari ya Songambele Simanjiro haujakamilika kwa zaidi ya miaka miwili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *