Mwili wa Askofu Castory Msemwa wa Jimbo Katoliki la Tunduru Masasi umeagwa leo jijini Dar es Salaam.

Askofu Msemwa alifariki dunia Oktoba 19,2017 mjini Muscat nchini Oman akiwa safarini kwenda India kwa matibabu.

Taarifa ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ilisema Askofu Msemwa alikuwa na tatizo la kiafya kwa kipindi cha miaka miwili na alikuwa akipata tiba na kuendelea na shughuli za kitume.

Akizungumza wakati wa ibada ya mazishi leo, Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi, Bruno Ngonyani amesema hali ya afya ya Askofu Msemwa ilikuwa imeimarika.

Amesema waumini na wananchi kwa jumla, wajipange kwa ajili ya safari ya mwisho kwa sababu hakuna anayejua siku wala saa.

Mwili wa Askofu Msemwa umesafirishwa leo Masasi ambako utazikwa kesho katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Francisco Xavery la Jimbo la Tunduru Masasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *