Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka waandishi wa habari kuandika habari kwa kutunza na kuheshimu mila na desturi za kiafrika.

Akuzungumza leo katika maadhimisho ya Siku ya Vyombo vya Habari Duniani ambayo kitaifa imefanyikia jijini Arusha, Rais Samia amesema kukopa mila na desturi husababisha migongano isiyo ya lazima.

Uhuru wa habari hauchagui mipaka hivyo pamoja na hilo waandishi wa habari wanatakiwa kuzingatia mila na desturi za kiafrika kuandika mazuri ikiwemo vivutio vyote vilivyomo.

Amesema ni vyema wakaandika habari ka kuthamini rasilimali zilizopo Afrika ni vyema kujivunia rasilimali mlizonazo pamoja na kuzilinda.

Katika maadhimisho hayo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeeleza kuridhishwa za ukuaji wa uhuru wa vyombo vya habari nchini na uhuru wa kujieleza.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi mkazi wa UNESCO Kanda ya Afrika ya Mashariki, Profesa Hubert Gijzenz amesema Tanzania ilistahili kuandaa maadhimisho hayo ambayo yameshirikisha wahabari kutoka mataifa 54 barani Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *