Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya Tanzania imedhamiria kuanzisha na kukuza viwanda ili kukidhi mahitaji ya wananchi.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa Duniani hii leo,Bi Samia amesema serikali itashirikiana na viongozi wa umoja wa kimataifa ili kuhakikisha changamoto  za uwekezaji zinatatuliwa .

Bi samia amelitaka shirika hilo kuweka uwazi na mabadiliko ya kweli katika baraza hilo na kwamba umoja wa mataifa ni watu na ni lazima wananchi wakafaidika na umoja huo.

Maadhimisho ya miaka 72 ya umoja wa mataifa yamefanyika kitaifa jijini Dar-es-salaam yakiongozwa na kauli mbiu isemayo maendeleo ya viwanda na utunzaji wa mazingira kwa maendeleo endelevu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *