Mwili wa Askofu Castory Msemwa wa Jimbo Katoliki la Tunduru Masasi umeagwa leo jijini Dar es Salaam.

Askofu Msemwa alifariki dunia Oktoba 19,2017 mjini Muscat nchini Oman akiwa safarini kwenda India kwa matibabu.

Taarifa ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ilisema Askofu Msemwa alikuwa na tatizo la kiafya kwa kipindi cha miaka miwili na alikuwa akipata tiba na kuendelea na shughuli za kitume.

Akizungumza wakati wa ibada ya mazishi leo, Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi, Bruno Ngonyani amesema hali ya afya ya Askofu Msemwa ilikuwa imeimarika.

Amesema waumini na wananchi kwa jumla, wajipange kwa ajili ya safari ya mwisho kwa sababu hakuna anayejua siku wala saa.

Mwili wa Askofu Msemwa umesafirishwa leo Masasi ambako utazikwa kesho katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Francisco Xavery la Jimbo la Tunduru Masasi.

 

Makamu wa rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya Tanzania imedhamiria kuanzisha na kukuza viwanda ili kukidhi mahitaji ya wananchi.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa Duniani hii leo,Bi Samia amesema serikali itashirikiana na viongozi wa umoja wa kimataifa ili kuhakikisha changamoto  za uwekezaji zinatatuliwa .

Bi samia amelitaka shirika hilo kuweka uwazi na mabadiliko ya kweli katika baraza hilo na kwamba umoja wa mataifa ni watu na ni lazima wananchi wakafaidika na umoja huo.

 

Maadhimisho ya miaka 72 ya umoja wa mataifa yamefanyika kitaifa jijini Dar-es-salaam yakiongozwa na kauli mbiu isemayo maendeleo ya viwanda na utunzaji wa mazingira kwa maendeleo endelevu.

 

 

 

 

 

 

 

Mwenyekiti wa mtaa wa Tanesco wilayani mbulu mkoani manyara Joseph Paul ametoa wito kwa wakazi wote wa mtaa huo kulinda mazingira yao.

Akizungumza na kituo hiki,Bw Paul ni vyema wananchi wakatunza mazingira yao hasa vyanzo vya maji ilikujikinga na milipuko ya magonjwa inayoweza kujitokeza.

Mwenyekiti ametoa rai hiyo baada ya mtu mmoja asiye julikana kujisaidia haja kubwa katika kisima cha maji wanachotumia wananchi kwa matumizi ya familia.

 

Bw Joseph amewaomba wakazi wote wa mtaa huo kuyalinda na kuyatunza mazingira yanayo wazunguka.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa mtaa huo wamelaani kitendo hicho na kuiomba serikali kuwashughulikia watu wote wenye tabia kama hizo katika jamii.

 

Wakazi hao wamewataka watu wote wenye tabia kama hizo kuachana nazo mara moja kwa ustawi wa mazingira yao.

 

======================

 

 

 

 

 

Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)  Profesa Eleuther Mwageni amesema wanafunzi wenye vigezo vya kujiunga na elimu ya juu wanatakiwa kuripoti chuoni Oktoba 30 ili kuanza masomo yao.

 

Prof.Mwageni ameyasema hayo leo wakati anatoa ufafanuzi juu ya tarehe ya kufunguliwa kwa vyuo kutokana na mkanganyiko ambao wameupata baadhi ya wanafunzi wanaojiunga na masomo kwa mwaka 2017/18.

 

Amesema,Tarehe ya Kalenda ya masomo haijabadilika ambayo ni Oktoba 30 nakwamba wanafunzi wanatakiwa kuanza masomo ya elimu ya juu kwa mwaka huo.

 

Aidha Prof. Mwageni amesema zaidi ya wanafunzi laki nne na Elfu hamsini tayari wameshapata vyuo na kwamba kinachosubiriwa katika awamu ya tatu ni kupitisha wanafunzi wengine elfu kumi na mbili ili kufikia malengo ambayo ni wanafunzi elfu hamsini na saba.

 

Mapema mwaka huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alishauri TCU iweke utaratibu wa wanafunzi kuomba nafasi chuoni moja kwa moja ili waende vyuo wanavyotaka wao tofauti na awali ambapo zoezi la kupanga vyuo lilikuwa linasimamiwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini.

 

==============

 Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amewataka wafuasi wake kutoandamana na badala yake kusalia majumbani mwao siku ya uchaguzi.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amewataka wafuasi wake kutoandamana na badala yake kusalia majumbani mwao siku ya uchaguzi.

”Hatujawaambia watu wafanye maandamano siku ya uchaguzi. Hatujasema hilo hata kidogo”, Odinga alisema siku ya Jumanne katika mahojiano na BBC.

Alhamisi iliopita , Bwana Odinga na upinzani wake wa Nasa uliwaambia wafuasi wao kujiandaa kufanya maandamano wiki ya Uchaguzi mkuu.

Lakini katika mahojiano, bwana Odinga alisema kuwa maoni yake ni tofauti na yale ya rais Uhuru Kenyatta ambaye amesisitiza kwamba ni lazima uchaguzi ufanyike katika kipindi cha siku 60 kama ilivyoagizwa na mahakama ya juu.

”Kuna kambi mbili hapa, wale ambao wanataka kushiriki katika uchaguzi usio huru na haki na wale ambao wanasema hapana sio sawa kufanya hivyo”, alisema Odinga.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Image captionRais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Baada ya Raila Odinga kushinda katika malalamishi yake aliyoiwasilisha mahakamani , tume ya uchaguzi ilichapisha tarahe 26 kuwa tarahe ya uchaguzi mpya baada ya mahakama ya juu kufutilia mbali ushindi wa rais Uhuru Kenyatta.

Lakini bwana Odinga aliwasilisha orodha ya masharti kwa tume ya uchaguzi ambayo alisema ni sharti yaafikiwe kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mpya ikiwemo kubadilishwa kwa kampuni itakayochapisha makaratasi ya kupigia kura, kampuni yenye mfumo wa kielektroniki ya kupigia kura, mbali na kushinikizwa kujiuzulu kwa afisa mkuu wa tume hiyo Ezra Chiloba pamoja na maafisa wengine wakuu wa tujme hiyo.

Wiki mbili kabla ya uchaguzi , bwana Odinga alijiondoa katika uchaguzi huo na kutaka uchaguzi mpya kufanyika baada ya siku 90 baada ya uteuzi kufanywa.

Lakini uamuzi wa mahakama kuu uliowaruhusu wagombea wengine wanane kushiriki katika uchaguzi huo ulimrudisha rais Odinga katika wagombea wanaofaa kushiriki katika uchaguzi, huku rais Uhuru Kenyatta akisema kuwa ni chaguo la Odinga kushiriki uchaguzi huo au la.

Katika mahojiano hayo bwana Odinga amelitaja kama jaribio la kuwatishia Wakenya hatua ya vigogo wa chama tawala cha Jubilee kuvalia magwanda ya kijeshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *