Mahakama ya juu nchini Kenya itatoa uamuzi wa muda wa mwisho kuamua iwapo marejeleo ya uchaguzi wa urais yanaweza kufanyika siku ya Alhamisi.
Mahakama hiyo itasikiliza ombi la dharura siku ya Jumatano kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafutiliwa mbali siku moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo.
Hatua hiyo inajiri baada ya mahakama hiyo kufanya uamuzi wa kihistoria ilipofutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais na kutaka uchaguzi huo kurudiwa.
Kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga ametumia mojawapo ya uamuzi wa mahakama kujiondoa katika uchaguzi huo akiutaja kuwa usio huru na haki na hautatoa maono ya Wakenya.
Rais aliyepo sasa Uhuru Kenyatta amesema kuwa uchaguzi huo ni sharti ufanyike, huku akiwa na muswada wa uchaguzi katika meza yake unaotarajiwa kutiwa saini
Mahakama ya juu imekubali kusikiliza ombi hilo la muda wa lala salama ambalo linahoji iwapo tume ya uchaguzi na mwenyekiti wake wataweza kufanya uchaguzi ulio huru na haki siku ya Alhamisi.