
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema maandalizi ya sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 23, 2022 hadi sasa yamefikia asilimia 81.
Majaliwa ameyasema hayo wakati wa sherehe za miaka 58 ya muungano wa Tanzania na Zanzibar.
Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watanzania kufanya maandalizi ya siku hiyo na kuwa tayari kuwapokea wataalam wa sensa nchini kwa ajili ya kuhesabiwa.
Amesema kuwa kwa lugha nyingine atakayeshindwa kuhesabiwa ni kujinyima fungu lako katika mipango ya maendeleo nchini kwa sababu sensa ni kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.