Watumiaji na Wanufaika wa Ziwa Babati Mkoani Manyara wameshauriwa kutumia Ziwa hilo kwa kufuata taratibu za utunzaji wa mazingira ili kuepuka uharibifu wa chanzo cha Maji na Samaki wanaopatikana katika Ziwa hilo.Ushauri huo umetolea na Afisa Misitu Mkoa wa Manyara  ambaye ni Msimamizi wa Mazingira Michael Gwandu wakati akiongea na kituo hiki. Amesema wakati Serikali ikiendelea na jitihada za kurudisha hadhi ya Ziwa Babati ameiasa jamii kutumia njia sahihi katika shughuli za uvuvi ili kuepuka athari zitakzojitokeza.

Licha ya  ziwa Babati kuwa  miongoni mwa vyanzo vya maji vilivyopo katika mkoa wa manayara na kuwanufaisha wananchi kutokana na  uvuvi limekuwa likiathiriwa na shughuli za binadamu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *