Kamati  ya ulinzi na usalama ya Wilaya Ya Biharamulo Mkoani Kagera imeapa kuhakikisha wafugaji wote ambao wamekaidi kuondoka katika mapori ya akiba yaliyoko katika wilaya hiyo wanakamatwa na kufunguliwa mashitaka kwa mjibu wa sheria ikiwemo kutaifisha mifugo yao.

Mwenyekiti  wa kamati hiyo ya ulinzi na usalama na mkuu wa wilaya ya Biharamulo Bi Saada Malunde ametoa kauli hiyo mara baada ya ziara iliyofanywa na kamati hiyo ili kuona kama wafugaji hao wanaondoa mifugo yao kwa hiari kabla ya zoezi la kuwaondoa kwa nguvu halijaanza kutekelezwa

Aidha  katika mapori hayo ambayo ni ya akiba inaaminika kuwa wapo baadhi ya wafugaji ambao ni raia wa kigeni wanaotumia raslimali ambazo zingewafaidisha watanzania lakini pia baadhi ya wafugaji nakusema kuwa agizo hilo litaendelea.

Kwa upande wake afisa uhamiaji wa wilaya ya Biharamulo, Bw Justin Kewisa amesema kuwa ofisi ya uhamiaji nayo itashiriki operesheni ya kuwaondoa wafugaji katika mapori hayo ya akiba kwa kuwa inaaminika kuwa wapo wafugaji ambao si raia wa Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *