Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro wameazimia kwa pamoja  kupitiwa upya kwa mchakato wa kuwepo kwa jiji la Moshi ambalo litahusisha baadhi ya vijiji wilayani humo.

Wakizungumza katika kikao cha Baraza hilo, baadhi ya madiwani wamesema hawajashirikishwa  pamoja na wanavijiji ambao wanatakiwa maeneo yao yajumuishwe kwenye uanzishwaji wa jiji la Moshi.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Michael Kilawila ametoa ushauri kwa wataalamu wa halmashauri hiyo juu ya mchakato wa uanzishwaji wa jiji la Moshi.

Hata hivyo Afisa Ardhi wa Wilaya ya Moshi, Cecilia Mwing’uri amesema vikao vyote vimefanyika kwa kuzishirika Halmashauri zote na tayari kibali cha serikali cha kuridhia uanzishwaji wa  jiji la Moshi kimeshatolewa.

Mchakato wa kuanzishwa kwa Jiji la Moshi utajumuissha kilomita za mraba 68 katika  Halmasshauri ya Moshi vijijini na kilomita za mraba 16  kutoka wilaya ya Hai.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *