Wananchi wilayani Mbulu mkoani Manyara wametakiwa kutokuwa na hofu yeyote baada ya wagonjwa wa kifua kikuu {TB}kuchanganywa katika wodi ya wagonjwa wengine katika hospitali ya wilaya hiyo.
Hayo yamesemwa na kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya Mbulu daktari Hhangali Qwaray wakati akizungumza na redio habari njema kuhusiana na baadhi ya wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo kulalamikia kuchanganywa katika wodi moja na wagonjwa wa kifua kikuu.
Aidha doktari Hhangali ameitaka jamii kuwa tabia za kupima afya zao mara kwa mara pindi waonapo dalili ya ugonjwa huu wa kifua kikuu ili kuzuia mambukizi kutoka kwa mtu mmoja ndani ya familia kwenda kwa mtu mwingine.
Hata hivyo daktari amehitimisha kwakuisisitizia jamii kuzingatia usafi wa mazingira , na kujenga nyumba ambazo zina madirisha ya kutosha na kuzingatia usafi binafsi kama kufunga mdomo kwa kitambaa wakati wakukohoa na kupiga chafya .