RAIS Dk. John Magufuli anatarajiwa kufungua kongamano la maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata).
Akizungumza kwa niaba ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Aboubakar Zuberi Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata, Sheikh Khamis Mataka, amesema kongamano hilo litafanyika Aprili 24.
Amesema lengo la kongamano hilo ni kujadili mmomonyoko wa maadili uliopo ndani ya jamii hivi sasa.
Amesema kongamano hilo la siku moja litafungwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Sheikh Mataka amesisitiza kuwa maadili ni muhimu ndani ya jamii na kwamba kwa sasa nchi inakabiliwa na mmomonyoko wa maadili.