Serikali imetakiwa kuboresha huduma katika vituo vya afya na hospitali za rufaa ili kupunguza msongamano katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na wagonjwa wengi kukimbilia hospitalini hapo.

Hayo yamebainishwa na daktari bingwa wa magonjwa ya akinamama Dkt. Geophrey Marandu kufuatia idadi kubwa ya wanawake wajawazito kujitokeza kupata huduma hospitalini hapo.

Dkt. Marandu ametoa wito kwa wagonjwa hususan akinamama kuzingatia lishe bora kwani hospitali hiyo inatoa huduma bora licha ya kuwepo kwa ongezeko kubwa la wagonjwa.

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ni hospitali kuu ya rufaa inayopokea idadi kubwa ya wagonjwa wanaohitaji huduma za rufaa kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *