Serikali Wilayani Kiteto Mkoani Manyara imeanza msako wa kuwasaka watoto ambao hawajapelekwa shuleni ili waweze kupatiwa haki yao ya kimsingi.
Katibu tawala wa Wilaya ya kiteto, Ndaki Stefano amesema kwa sasa wamepata mafanikio makubwa zaidi kuwapata wanafunzi ambao wazazi wao wamewazuiya kuendelea na masomo huku akitoa wito kwa jamii kuhakikisha kuwa wanapeleka watoto wao shule jambo ambalo ni haki yao ya msingi na ya kikatiba.
Ndaki amefafanua kuwa oparesheni hiyo imeanza na ni endelevu ambapo imeanzia katika kijiji cha ndiligishi.
Aidha ameongeza kuwa njia pekee ya kutoa haki kwa watoto ni kuwapatia elimu ili baadaye waweze kujimudu katika maisha yao.
Pia wananchi wamesema kuwa hatua hiyo ni nzuri ambayo serikali inafanya kwani njia pekee ya kuwa na kizazi kilicho na elimu na kuweza kuendesha maisha yao.