Wanaume na wanawake wametakiwa kushirikiana katika vikundi vya vikoba ili kujiimarisha kiuchumi .

Kauli hiyo imetolewa na wananchi katika kata ya BASHNET walipokuwa wakipozungumza baada ya kutembelewa na idara ya jinsia na maendeleo jimbo katoliki la mbulu pamoja na mwakilishi wa baraza la maaskofu katoliki Ujerumani.

Mtoa Elimu katika Vikundi vy kukopa na kuweka katika kata hiyo Anjela Pius amewaomba wanawake kusimama imara katika kusimamia miradi yao bila ya kushindwa ili kueleka Tanzania ya viwanda.

Naye mratibu wa idara ya jinsia na maendeleo jimbo katoliki la mbulu BI: ANSILA TEMBO alipowatembelea wanafunzi wa shule ya mssingi Long amewaomba kuwa mfano kwa kutoa elimu kupinga ukatili wa kijinsia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *