Jumla ya watoto 269 wenye umri chini ya miaka mitano hufariki dunia kila siku nchini.

Pia  wajawazito 556 hufariki dunia pia kutokana na matatizo ya uzazi.

Hayo yamesemwa leo mjini hapa na mwakilishi wa shirika linalohudumia watoto duniani, (UNICEF), Maniza Zaman kwenye mkutano wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) unaofanyika mjini Moshi.

Zaman amesema kwa mujibu wa utafiti walioufanya, kwa upande wa  elimu, asilimia 39 tu ya watoto wa kike na kiume ndiyo wanaohitimu elimu ya sekondari nchini kila mwaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *