Serikali imeahidi kutopoke amradi wa bara bara ya Manyara- Dodoma  inayojengwa kwa kiwango cha lami endapo mkandarasi atashindwa kutimiza ujenzi kwa kiwango kama walivyokubaliana kwenye mkataba wao.

Akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Manyara Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa lengo la kutembelea ujenzi huo  mara kwa mara ni kuhakikisha Mkandarasi anafanya kazi yake kwa kiwango kinachokubalika.

Profesa Mbarawa ameeleza kwamba barabara hiyo inayoanzia Bonga –Mela yenye urefuwa kilomita 88.8 iliyogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 83.3 mpaka sasa imeshakamilika kwaasilimia 76 na kwamba kimebaki kipande chenye urefu wakilomita 18 kwaupandewaManyara.

Aidha amefafanua kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha barabara hiyo inakamilika baada ya miezi sita (6) na ifikapo mwezi Octoba mwaka huu kuzinduliwa rasmi na kuongeza kuwa ni jukumu la wananchi kuhakikisha wanaweka ulinzi wa kutosha baadaya barabara hiyo kukamilika.

Pia ametoa shukrani kwa Tanroads kwa mikoa hiyo pamoja na Mkandarasi kwa ujenzi ambao unaonyesha utakamilika kwa wakati unaotakiwa na ambao upokatika viwango vinavyokubaliwa, hivyo wananchini bora wakailinda kwanini kilio chao cha muda mrefu.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wadaraja la Magara linalounganisha wilaya za Mbulu na Babati alisema Zabuni ya kumpata mkandarasi wa ujenzi wa daraja hilo inatarajiwa kufunguliwa tarehe 28 mwezi Aprili ambapo tayari serikali imekwishatenga malipo ya awali kwa ajili ya malipo ya mkandarasi atakaepatikana.

Katika bajeti 2017/2018 serikali itahakikisha inatengafedha zakukamilish aujenziwadaraja hiloambalo ni muhimu nategemezi kwa wakazi wawilaya zotembili na watalii wanaoingia katika hifadhi ya ziwa Manyara.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Dokta Joel Bendera alisema kuwa mkoa utaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha mkandarasi anakamilisha kazi hiyo kwa wakati na viwango vitakavyokubaliwa katika mkataba wa kazi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *