mga

Zimbabwe inasherehekea miaka 37 tangu kupata uhuru chini ya rais Robart Mugabe  mwenye unmri wa miaka 93.

Maadhimisho hayo yanafanyika kipindi ambacho Zimbabwe inakabiliwa na kushuka thamani kwa pesa yake hatua iliyosabisha  wizara ya elimu nchini humo kutangaza ada zilipwe kwa mfumo wa mifugo.

Katibu mkuu wa wizara hiyo, Sylvia Utete-Masango alinukuliwa na vyombo vya habari akisema wameandaa mfumo kwa wanafunzi kutoa mifugo kama ada kwa maeneo ya vijijini huku mijini wazazi watatakiwa kufanya  vibarua maalum mashuleni ili kufidia ada za watoto wao.

Rais Mugabe ameiongoza Zimbabwe tangu ilipopata uhuru wake mwaka 1980.

Viongozi mbalimbali duniani wametuma salama za pongezi kwa nchi hiyo akiwemo rais wa Russia,  Vladimir Putin na malkia wa Uingereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *