Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatazamia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu ya Royal Tour itakayofanyika leo tar 28/4/2022 katika ukumbi wa Kimataifa AICC Mkoani Arusha
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela amesema kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa na kuwataka wananchi kujitokeza kumpokea.Rais anzia uwanja wa ndege wa Kia.
Kwa Upande wake Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo alisema kuwa wageni wote wasiwe na hofu ulinzi umeimarishwa
Aidha Masejo amesema kutokana na tukio la Kitaifa hivyo Jeshi la Polisi nchini kwa Kushirikiana na Kamati ya Usalama mkoa imehakikisha kuwa hali ni shwari na kila raia anakuwa salama.