
Rais samia suluhu ameeleza mafanikio yaliyopatikana katika safari yake nchini marekani, ikiwepo kusaini mikataba na wawekezaji yenye thamani ya sh trilioni 11.7.
akizungumza leo baada ya kuwasili nchini na ndege ya qatar airways katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (kia), rais samia amewataka watanzania kujiandaa kuwapokea wawekezaji hao wakija nchini.
rais samia amesema wawekezaji hao kama wakija nchini, wanatarajiwa kutoa ajira kwa watu laki tatu na elfu moja [301,000.]
kuhusu sekta ya utalii amesema baada ya kuathirika na uviko-19 sasa watalii wameanza kuongezeka sambamba na mapato.
amesema watalii wameongezeka kutoka 620,866 mwaka 2020 hadi 922,692 mwaka 2021 na mapato kutoka dola 714 milioni hadi dola 1,254 milioni mwaka 2021.