Imelezwa Kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar imeleta faida kwa Tanzania hasa umoja wa kitaifa, upatikanaji wa ajiri pamoja na ulinzi imara.
Hayo yamesemwa na Afisa Uchaguzi Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mkoani Manyara alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Rada katika maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano .
Naye Mwalimu James Kaijage wa Kanisa la Kkkt Mbulu Mjini ametoa wito kwa viongozi wa dini kuombea muungano huu ili uzidi kudumu na kuwanufaisha Watanzania .
Maadhimisho ya miaka 58 ya muungano wa Tanganyika na zanzibara yamefanyika kitaifa Jijini Dodoma ambapo yamebeba kauli mbiu isemayo, miaka 58 ya Muungano uwajibikaji na uongozi bora tushiriki katika Sensa ya watu na makazi kwa maendeleo yetu.