waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka Wafanyabiashara wa pande zote mbili za Muungano watumie vyema fursa ya kibiashara ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili wajengane kibiashara kabla ya kufikiria kutoka nje.
Amesema kuwa mbali na kuwa na soko kubwa la watu zaidi ya milioni 60 ndani ya Muungano pia kuna soko kubwa zaidi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo mwezi uliopita tu waliikaribisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuwa mwanachama.
Waziri Mkuu ameyasema hayo alipomuwakilisha Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango katika Ufunguzi wa Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanzania, yaliyofanyika katika uwanja wa Maisara, Zanzibar.
Aidha, Waziri Mkuu amewataka Watanzania waendelee kujivunia na kuyatangaza mafanikio na maendeleo makubwa yanayotokana na kasi ya viongozi wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Dkt. Hussein Ally Mwinyi, Rais wa Serika la Mapindizi ya Zanzibar

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *