Wilaya ya Mbulu mkoani manyara  inatarajia kuwapatia chanjo  ya polio  kwa  watoto  77,000[elfu sabini na saba ]   ili kuwakinga na ugonjwa wa polio.

Akizungumza na kituo hiki Mkuu wa wilaya ya Mbulu  Sezaria Veneranda Makota  amesema Wilaya ya Mbulu tayari imeshafanya maandalizi kwaajili ya kutoa chanjo hiyo ya polio itakayofayika nyumba kwa nyumba kwa kuwashirikisha viongozi wa mitaa na vijiji.

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu amewasihi wananchi kuwapa ushirikiano wataalamu wa afya na viongozi watakaokuwa wanatoa chanjo hiyo ili zoezi hilo lifanikiwe kwa kiasi kikubwa.

Akielezea ugonjwa wa polio Mratibu wa chanjo ya polio kwa Halmashauri ya Mji wa Mbulu  Edward Misana amesema  ugonjwa huo unasababishwa na kinyesi chenye virusi  vya ugonjwa huo.

Chanjo ya polia inatarajiwa  kutolewa tr 28-4-2022 hadi tr 1-5-2022 kwa nchi nzima ambapo watoto wenye umri kuanzia miaka sifuri hadi mitano wanatarajiwa kupata chanjo hiyo  na hii ni kutokana na tr 12-2-2022 mtoto mmoja mwenye ugonjwa wa polio kugunduliwa nchini Malawi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *