
Rais wa zamani wa Kenya Mwai Kibaki amefariki dunia, akiwa na umri wa miaka 90.
Katika taarifa yake, Rais Kenyatta aliyepokea kijiti kutoka kwa mzee Kibaki amesema kiongozi huyo ataandaliwa mazishi ya kitaifa huku akitoa pole kwa wakenya katika kipindi hicho cha maombolezo.
Rais Kenyataa amesema Taifa hilo litamuenzi mzee Kibaki kwa mchango wake katika taifa hilo ikiwamo upatikanaji wa katiba mpya ya mwaka 2010, mageuzi katika ukuaji wa kiuchumi, demokrasia na kuimarisha hali ya uchumi ya Wakenya.
Rais Uhuru Kenyatta ametoa agizo la kufanyika maombelezo ya kitaifa ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti.