Mwanaume mmoja Elisha Ntai mkazi wa kitongoji cha Manyara kijiji cha Gedamara wilaya ya Babati mkoani Manyara amefariki dunia baada ya kukatwa kwa panga kichwani.
Paulo Chepa Mwenyekiti wa kijiji cha Gedamara kata ya Galapo amesema tukio hilo limetokea April 16,2022 saa tatu usiku.
Chanzo cha Mauaji ni ugomvi wa kifamilia ambapo marehemu alikuwa akijaribu kuokoa ugomvi wa watoto waliokuwa wakipigana.

Ndugu wa marehemu  Bwana Emanueli Nada Gwandu anaeleza ameeleza kuwa ndugu  yake ambaye ni mtoto wa shangazi yake amefariki baada ya kufikishwa hospitali ya mkoa kwa ajili ya matibabu
Amesema tayari mtuhumiwa amekamatwa kwani baada ya kutenda tukio hilo alitoroka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *