
Madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri wametakiwa kutumia nauli elekezi zilizotolewa na latra na kuacha tabia ya kuapndisha nauli kiholela kwa kusingizio cha kupanda kwa bei ya mafuta.
Hayo yamesemwa na afisa mfawidhi wa latra mkoa wa manyara joseph zongwe …alipokuwa akizungumza na kitoa hiki kwa njia ya simu ambapo amewataka wasafiri kutoa taarifa pale wanapobaini kupandishiwa nauli.
Amesema kuwa mamlaka yenye uwezo wa kupandisha nauli ni mamlaka ya usafirishaji nchi kavu Latra na hivyo watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.
Hivi karibuni baadhi ya maredereva wamekuwa na tabia ya kutoza nauli ya juu kwa kusema kuwa mafuta yamepanda bei.