Wazazi na walezi wameshauriwa kuzingatia haki za watoto ikiwa pamoja na kuwapa malezi bora ili kujenga Taifa lenye kizazi chenye maadili mema.
Ushauri huo umetolewa na Afisa Ustawi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Bwana Tomas Simbeye wakati akiongea na kituo hiki na kuwaasa wazazi kuacha tabia ya kuwafanyisha kazi ngumu watoto.
Aidha,Bwana Simbeye amesema watoto hawapaswi kupewa majukumu ya kazi ambayo yatasababisha kuathiri afya zao au hatua za ukuaji .
Katika hatua nyingine,amesema kuwa mtoto chini ya umri wa miaka 14 anapaswa kufanya kazi nyepesi ambazo hazitakiwi kuzidi masaa 6 kwa siku.