Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Media Foundation Bi Fausta Musokwa amevitaka Vyombo vya Habari vinavyofadhiliwa na TMF kufanya kazi kwa Kuzingatia Ubora wa Vipindi,Mikakati ya Upatikanaji na Matumizi ya Fedha na Utawala Bora ili kuvifanya Vyombo hivyo Vijisimamie kiuchumi na Kuwa Mfano kwa Vyombo vingine Vya habari ambavyo Haviko kwenye Mradi.
ameyasema hayo jijini dodoma katika warsha ya siku tano iliyoanza tarehe 14.5.2018 hadi tarehe 17.5.2018kati ya taasisi hiyo na vyombo vya habari vilivopewa miradi na TMF. Vyombo hivyo ni Radio Habari Njema kutoka Manyara,CG FM kutoka Tabora,standard FM Kutoka mkoani Singida ,Gazeti la Jamhuri,Zanziber leo,Kili FM Kutoka Kilimanjaro,Ebony FM kutoka Mkoani Iringa