RAIS MAGUFULI AOMBWA KUIKABIDHI SIMBA SC KOMBE JUMAPILI TAIFA

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema kwamba amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli kuwakabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu, Simba SC Jumapili Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya ofisi za TFF, Uwanja wa Karume, Ilala mjini Dar es Salaam, Karia amesema kwamba wanasubiri majibu kuhusu ombi hilo.
Pamoja na hayo, Rais Karia amesema kwamba siku hiyo kama Rais Magufuli atakubali mwaliko huo, ataanza kwa kukabidhiwa Kombe la ubingwa wa michuano ya Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (CECAFA U17), ambalo Tanzania ilitwaa mapema mwezi huu nchini Burundi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *