Jamii imeshauriwa kuwa makini na kuzingatia elimu inayotolewa na jeshi la zima moto na uokoaji katika utumiaji wa majiko ya gesi kwenye familia ili kupunguza majanga ya moto yanayoweza kujitokeza.
Ushauri huo umetolewa na Afisa habari na mahusiano kwa umma ofisi ya kamanda wa jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa Manyara Sajent Chande Abdalah wakati akizungumza na kituo hiki .
Aidha amesema baadhi ya majanga ya moto yanasababishwa na kutokua makini ma Vifaa vya umeme pamoja na gesi.
Aidha,Sajent Chande amesema watumiaji wa gesi wanapaswa kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kukagua , kubadilisha mipira inayopitisha gesi na kufunga majiko ya gesi vizuri mara baada ya kuyatumia.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua kitabu cha Historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kitakachozinduliwa tarehe 26 Aprili, 2022 siku ya kilele cha Maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano huo.
Baada ya uzinduzi, Ofisi ya Makamu wa Rais imepanga kuwa na mpango endelevu wa kutoa elimu kwa umma kuhusu historia ya Muungano na masuala ya msingi kuhusu Muungano
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo amesema Muungano unapotimiza miaka 58 ni jambo la kujivunia na kuendeleza mazuri yaliyopatikana kutokana na Muungano.
Amesisitiza kuwa maadhimisho ya Muungano kwa mwaka huu yataambatana na matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuelimisha umma kuhusu historia ya Muungano, ulipotoka, ulipo na unapoelekea
Serikali imekiri kuwa na taarifa kuhusu jiwe la rubi lenye uzito wa kilo 2.8 ambalo linatajwa kuwa linatoka Tanzania lakini bado haijathibitika.
Hayo yamesemwa bungeni na Naibu Waziri wa Madini, Dk Stephen Kiruswa alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Mkinga, Dustan Kitandula.
Dk Kiruswa amesema Serikali ilipata taarifa za uwepo wa jiwe hilo tangu Aprili 13,2022 na kwamba, lina thamani ya dola 120 milioni za Marekani sawa na Sh240 bilioni za Tanzania.Taarifa zinasema litawekwa sokoni ndani ya siku 30 baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Deus Seif amesema Walimu walionufaika kwa kupandishwa madaraja (vyeo) katika kipindi cha mwaka 2021/2022 pekee ni 92.9% ya Walimu wote ambao ni takribani 260,000.
Deus ametoa kauli hiyo akiwa Jijini Mwanza ambapo amesema Ajira imetolewa kwa awamu nne, ya kwanza Walimu 13,000, ya pili 7000, ya tatu 6000 na ya nne ni 12,000 ambayo ni sawa na 15% ya Walimu waliopo.
Kwa upande wa madaraja (vyeo) mwaka jana Walimu 127,000 wamepanishwa vyeo, mwaka huu zajdi ya 60,000, watakaonufaika na kupandishwa daraja ni Walimu 52,0000 ambapo jumla ya walionufaika ni sawa na 92.9%
Aidha amesema kuwa serikali imeboresha miundombinu ya madarasa/samani na vitabu na kwa sasa TAMISEMI imeanza zoezi la ujenzi wa nyumba za Walimu.
UNAENDELEA KUSIKILIZA TAARIFA YA HABARI KUTOKA REDIO HABARI NJEMA ZIFUATAZO SASA NI HABARI ZA KIMATAIFA;
Rais wa China Xi Jinping ameupendekeza mpango wa usalama duniani ambao unaheshimu kanuni ya usalama usiotenganishwa, ambao ni wazo lililoiidhinishwa pia na Urusi.
Katika mkutano wa kila mwaka wa Jukwaa la Boao Asia, Xi amesema kuwa ulimwengu unapaswa kuheshimu uhuru na mamlaka ya mipaka ya nchi zote, wakati ukizingatia masuala halali ya usalama wa wote.
Katika mazungumzo kuhusu Ukraine, Urusi imesisitiza kuwa serikali za Magharibi ziheshimu makubaliano ya mwaka wa 1999 yanayozingatia kanuni ya usalama usiotenganishwa, kuwa hakuna nchi inayoweza kuimarisha usalama wake kwa gharama ya wengine.
China na Urusi zimeimarisha mahusiano yao, na China imekataa kuulaani uvamizi wa Urusi wa Februari 24 nchini Ukraine, ambao Moscow inauita kuwa ni operesheni maalum ya kupunguza nguvu za kijeshi za nchi hiyo.
Italia imesaini mkataba na Angola wa kuongeza usambazaji wa gesi kutoka nchi hiyo ya kusini mwa Afrika wakati ikipambana kuwachana na gesi ya Urusi kuhusiana na vita vya Ukraine.
Taarifa kutoka kwa waziri wa mambo ya kigeni wa Italia Luigi Di Maio imesema kuwa mkataba huo unathibitisha dhamira ya Italia ya kuwa na vyanzo mbadala vya usambazaji wa nishati.
Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi anataka kuiongeza Angola na Congo-Brazzaville kwenye orodha ya wauzaji wa gesi nchini Italia, kuchukua nafasi ya Urusi, ambayo husambaza asilimia 45 ya gesi inayotumika Italia kwa wakati huu.
Waziri Di Maio ameandamana na mwenzake wa Ikolojia Roberto Cingolani katika ziara ya Angola na wameendelea Congo-Brazaville ambapo watakutana na Rais Denis Sassou Nguesso.
KABLA YA KUMALIZA TAARIFA YA HABARI, HUU TENA NI MUHTASARI WAKE;
Jamii imeshauriwa kuzingatia elimu inayotolewa na jeshi la zima moto na uokoaji katika utumiaji wa majiko ya gesi ili kupunguza majanga ya moto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua kitabu cha Historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili, 2022.
na katika habari za kimataifa, Rais wa China Xi Jinping ameupendekeza mpango wa usalama duniani ambao unaheshimu kanuni ya usalama usiotenganishwa na nchi zote.
HIVI PUNDE MSIKILIZAJI TUNAKULETEA UCHAMBUZI WA HABARI ZETU NA ENDELEA KUTUSIKILIZA
MTANGAZAJI: Karibu msikilizaji katika uchambuzi wa Habari zetu ambapo tunazichambua Habari hizi kwa kina zikiwa zinasimuliwa na waandishi wetu.
Katika uchambuzi huu pia tunakuletea Habari za Uchumi na Biashara bila kusahau Habari za michezo na Burudani.
Nawe msikilizaji unayo nafasi ya kuchangia kwa kile utakachokisikia. Tuandikie ujumbe mfupi wa maandishi kwenda namba 0689 87 77 17.
Kwa niaba ya timu nzima ya chumba cha Habari, Mimi ni
UCHAMBUZI:
Mtangazaji: Jeshi La Zima Moto na Uokoaji Mkoa Wa Manyara limesema linaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kudhibiti majanga ya moto yanayoweza kujitokeza,
Mwanahabari wetu Epifania Magingo amefanya mahojiano na Afisa habari na mahusiano kwa umma ofisi ya kamanda wa jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa Manyara Sajent Chande Abdalah ameanza kwa kueleza hali ya majanga ya moto kwa mkoa wa Manyara ikoje…
Mtangazaji: serikali imesema itaendelea kukarabati barabara na kuzitengeneza kwa kiwango cha lami ili kurahisisha huduma kwa wananchi.
Hayo yamesemwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Godfrey Kasekenya alipokuwa akijibu maswali ya wa Bunge kuhusu matengenezo ya barabara ambapo pia barabara za mbulu , karatu ,Babati nazo zimezungumziwa.
Mtangazaji: Ni sauti ya Naibu Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Godfrey Kasekenya alipokuwa akijibu maswali ya wabunge kuhusu ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami.
MTANGAZAJI: Hii ni Redio Habari Njema ikitangaza kutoka MBULU mkoani Manyara na huu ni uchambuzi wa Habari zetu. Nawe msikilizaji unayo nafasi ya kuchangia katika yote unayoyasikia kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwenda namba 0689 87 77 17.