Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padri Raymond Saba amesema Ijumaa Kuu ni siku muhimu ambayo waumini wa kanisa hilo wanakumbuka fumbo la ukombozi kupitia mateso ya Yesu Kristo.

Ijumaa Kuu huadhimishwa siku moja kabla ya Sikukuu ya Pasaka (kufufuka kwa Yesu),  hivyo leo Wakristo dunia wanmeadhimisha siku hiyo.

Pasaka huadhimishwa ikiwa ni kumbukumbu ya mateso ya Yesu, huku viongozi wa dini wakihimiza upendo, msamaha na utu wema

Amesema Pasaka inaonyesha jinsi Mungu alivyo na upendo uliomuwezesha kumtoa mwanaye mpendwa Yesu Kristo kuteswa kwa kupigwa, kubebeshwa msalaba, kuvalishwa taji la miba na kutobolewa na mkuki hadi kufa ili kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *