Akizungumza katika mkutano wa baraza la madiwani Bw Mnyenye amesema wazazi wengi wanasababisha wanafunzi kupata mimba kutokana na kupoteza ushahidi pale mtuhumiwa anaposhitakiwa.
Kwa Upande wake Afisa elimu sekondari Bw: papa king kaai amesema serikali itachukua hatua kwa mtu yeyote atakaye husika kupoteza ushahidi.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya karatu Bw Abbas amesema suala la mimba ni la jamii nzima wala si mzigo wa serikali pekee.
Suala la mimba limekuwa tatizo kubwa linalochangia kukwamisha malengo ya wanafunzi wilayani Karatu kwa kukatisha masomo yao kutokana na Ujauzito.