Akizungumza  na kituo hiki Muuguzi kutoka hospitali ya mjii wa mbulu Bi. Anna Bonifasi  amesema ni vyema serikali iangalie hali ya  kuongeza wakunga katika hospitali  kwani ni wao ni wachache suala linalowafanya wafanye kazi kwa ziada.

Bi Boniface, Amesema Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yanatarajiwa kufanyika hapo kesho huku kwa wilaya ya mbulu na Kimkoa yanatarajiwa kufanyika tarehe 12 mwezi wa Tano Mwaka huu katika Hospitali ya Hydom.

Wakunga na wauguzi Siku hiyo watarudisha viapo vyao  na kufanya tendo la huruma kwa kuwapa pole wagonjwa pamoja na kufanya usafi kwenye mazingira yao.

=============

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *